Simba Vs Yanga #Live 16-04-2023 | NBC Premier League

Tazama
Yanga na Simba Live Kupitia Youtube, Matchday Live: Simba vs Yanga Tazama Moja kwa Moja Hapa

Baada ya takribani wiki nzima, mzizi wa fitna unaenda kukatwa katika dimba la Benjamin Mkapa leo wakati Simba na Yanga zitakapokutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC. Mchezo huo una umuhimu wa kipekee kwa kila timu na pengine hiyo inaweza kuwa sababu ili kuongeza ushindani

Simba wakiwa wenyeji wa mchezo huo watatoka rasmi kwenye mbio za ubingwa endapo watapoteza

Ushindi kwao hautamaanisha kurejea kwenye mbio za ubingwa kwa asilimia 100 pia kwani bado watakuwa na deni la pointi tano dhidi ya Yanga.

Ili wawe mabingwa, watalazimika kuiombea Yanga bahati mbaya katika mechi nne zilizobaki, wakati lazima washinde mechi zote.

Kwa Yanga ushindi dhidi ya Simba leo utawapa imani ya kutetea ubingwa wao kwa msimu wa pili mfululizo

Endapo Yanga itashinda leo, itahitaji pointi mbili pekee katika mechi nne zilizosalia ili kurejesha taji hilo Jangwani kwa mara ya 29.

Loading